Weka mipangilio ya nyumba yenye vifaa mahiri iliyopangiliwa na iliyowekewa mapendeleo ukitumia programu ya Google Home. Tumia programu ya Google Home kuweka mipangilio na kudhibiti vifaa vyako vya Google Nest, Wifi na Chromecast, pamoja na maelfu ya vifaa mahiri vya nyumbani vinavyooana kama vile taa, kamera, virekebisha joto na vinginevyo.
Wekea mapendeleo dashibodi yako ya mipangilio ya nyumba.
Bandika vifaa, mifumo otomatiki na vitendo vingine unavyotumia sana kwenye kichupo cha "Ninavyopendelea" ili uweze kuvifikia kwa urahisi mara tu unapofungua programu. Angalia mipasho yako ya moja kwa moja ya Kamera ya Nest na kengele ya mlango na uchanganue kumbukumbu ya matukio kwa urahisi. Weka mipangilio na udhibiti Ratiba kwenye kichupo cha Uwekaji Otomatiki. Na ubadilishe ruhusa zozote kwa haraka kwenye kichupo cha pamoja cha Mipangilio.
Fahamu kwa haraka matukio yanayoendelea nyumbani.
Programu ya Google Home imebuniwa ili ikuonyeshe hali ilivyo nyumbani kwako na kukuarifu kuhusu mambo ambayo huenda umeyakosa. Ingia nyumbani kwako wakati wowote na uone muhtasari wa ya hivi karibuni.
Dhibiti nyumba yako ukiwa popote.
Programu ya Google Home kwenye Wear OS hukuruhusu kudhibiti vifaa mahiri vya nyumbani vinavyooana kupitia saa yako. Washa taa, rekebisha kirekebisha joto au upate arifa kunapokuwa na mtu au kifurushi kwenye mlango wako wa mbele. Tumia kigae cha vipendwa au weka kifaa kwenye sura ya saa yako ili urahisishe mchakato wa kudhibiti nyumba yako kuwa sawa na kugusa saa yako.
Nyumba inayokufaa ni nyumba yenye faragha.
Mchakato wa kulinda faragha yako unaanza kwa mojawapo ya miundombinu bora zaidi ya usalama duniani, ambayo tunaijumuisha moja kwa moja kwenye bidhaa za Google ili ziwe salama kwa chaguomsingi. Na Google hutumia vifaa vyako oanifu pamoja na data yako ili kufanya nyumba yako ikufae, lakini inatumia mipangilio uliyoiruhusu pekee. Tembelea Kituo cha Usalama cha Google Nest katika safety.google/nest ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyolinda taarifa zako na kuheshimu faragha yako.
* Huenda baadhi ya bidhaa na vipengele visipatikane kwenye maeneo yote. Unahitaji vifaa vinavyooana.
Ilisasishwa tarehe
8 Mei 2025